Jeshi la Polisi Kigoma,limelazimika kutumia nguvu na
mabomu ya machozi kuwatawanya mamia ya wakazi wa mtaa wa katosho na kahabwa
kata ya kibirizi katika manispaa ya Kigoma ujiji ,waliokuwa wakiandamana
kupinga nyumba zao kuwekwa notisi ya kuhama kupisha ujenzi wa bandari kavu.
Hatua hiyo ilikuja baada
ya maafisa wa manispaa kuanza kutoa notisi za kuhama ifikapo mwisho wa mwezi
huu kwa zaidi ya kaya elfu moja na mbili ambazo tayari zimekwishalipwa zaidi ya
shilingi bilioni 12 kama fidia, hali iliyofanya wananchi wapinge na kuanza
maandamano ambapo wameeleza kuwa hawaridhiki na fidia iliyotolewa na mamlaka ya
bandari hivyo hawataondoka mpaka pale serikali itakapowafanyia tathmini upya na
kuwalipa kulingana na hali ya uchumi wa leo ili waweze kuhamia na kujenga
sehemu nyingine tofauti na hali ilivyo sasa ambapo fedha walizopewa hazitoshi
ununuzi wa kiwanja na kujenga.
Kwa upande wake kaimu
mkuu wa bandari kigoma yudas sukanyi amesema, kazi ya tathmini nyumba katika
eneo la kahabwa ilifanywa na manispaa na wao wamekwishatoa pesa zote
kulingana na tathmini iliyofanywa na wataalam wa manispaa na wanachosubiri ni
eneo hilo liwe wazi ili kazi ya ujengaji wa bandari ya nchi kavu ianze




0 comments:
Post a Comment