Watu watatu wamefariki dunia na sita kujeruhiwa
kwenye ajali iliyo husisha basi la saibaba lenya namba za usajili T720 ADE na lori la mizigo aina ya Mitsubishi CANTER T
742 CRS zilizo gongana uso kwa uso
katika eneo la sakina jijini arusha.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa tukio
limetokea majira ya saa tisa usiku wa leo wakati basi la saibaba likiwa
kwenye majaribio kutoka arusha kuelekea ngara mtoni na lori likiwa linatokea
oldonyo sambu kwenda arusha likiwa limebeba karoti ndipo basi linalodaiwa kuwa
mwendo kasi likapanda tuta kisha taa zikazimika na kupoteza mwelekeo na
kugongana uso kwa uso.
Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoa
wa Arusha liberatus Sabas amethibisha kutokea kwa ajali hiyo na kwataja waliyo
fariki na kuwa dereva wa basi athumani saidck anashikiliwa na jeshi la polisi.
Wakati huo huo jitihada za kuokoa miili ya watu
waliyo fukiwa na kifusi kwenye mgodi ya tanzatine one mererani zinaendelea na
mwili mmoja wa mtu aliye fariki dunia aliyejulikana kwa jina la saidi mgosi
umepatika huku waokoaji wakieleza hali ngumu iliyopo chini ya mgodo na mchimbaji
aliyenusurika gidesh benedict akakiri kumtambua na kueleza ilivyo kuwa.



0 comments:
Post a Comment