Serikali imewahakikishia watumishi wote katika sekta
ya Afya kuwa imejipanga kuhakikisha inashughulikia changamoto zote
zinazowakabili ndani ya sekta ya Afya huku ikiwataka kufanya kazi kulingana na
matakwa ya viapo walivyoapa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu
Waziri wa Afya Dkt Khamis Kigwangala,ambapo licha ya kuahidi kutoa ushirikiano
wa kutosha kwa chama cha madaktari wa kinywa na meno TDA, amewataka wataala hao
kuzidi kutoa elimu ya kutosha kwa jamii kuhusu magonjwa ya kinywa na meno, huku
akiwataka watalaamu wote kuhakikisha wanalinda misingi ya taaluma zao.
Katika hutuba ya rais wa chama cha madaktari wa afya
ya kinywa na meno TDA,Dkt Lorna Carneiro amebainisha kuwa miongoni mwa shughuli
zitakazofanyika kuelekea kilele cha maadhimisho hayo mach 20 mwaka huu mkoa
morogoro ni pamoja na utoaji wa elimu ya kinywa na meno katika shule za
mahitaji maalum zikiwemo za mtoni maalum, Sinza Maalum,Buguruni Maalum.
Watalaam wa afya ya kinywa na meno wanasema zaidi ya
asilimia 30 ya watoto wenye miaka 12 wanakabiliwa na tatizo la meno kutoboka,
huku asilimia 50 ya watoto wenye umri wa kubadilisha meno nao wakikabiliwa na
changamoto hiyo.
Awali uzinduzi huo wa wiki ya kitaifa ya afya ya
kinywa na meno ulitanguliwa na matembezi yaliyoongozwa na naibu huyo waziri wa
afya, maendeleo ya jamii, wazee na watoto na kuhudhuliwa na madakatari na wadau
mbalimbali wa afya ya kinywa na meno.


0 comments:
Post a Comment