Jeshi la polisi jijini Mwanza limelazimika
kuimarisha ulinzi wa hali ya juu baada ya wafuasi wa CHADEMA kufurika katika
Mahakama kuu jijini Mwanza wakifuatilia kesi ya ubunge ya aliyekuwa Mbunge wa
Nyamagana Ezekiel Wenje.
Inaelezwa kuwa shughuli mbalimbali za kijamii na
uchumi zilisimama kwa muda wa saa mbili kufuatia wingi wa wafuasi wa CHADEMA
kuwepo Mahakamani hapo.
Kesi hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu 2015 kati
ya aliyekuwa Mbunge wa zamani Ezekia
Wenje jimbo la Nyamagana na Mbunge wa sasa Stanslaus Mabula kesi hiyo
ilisimamishwa kuanzia saa 6 mpaka 8, ndipo mahakama iendelee kusikiliza
mashahidi wa upande wa Wenje.
Tutaendelea kukufahamisha kinachoendelea,Toa maoni
yako hapo Chini.



0 comments:
Post a Comment