Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza waziri wa
Kilimo na Mifugo Mwiguli Nchemba kuwanyang’anya vitalu vya ufugaji wawekezaji
walivyomilikishwa na kampuni ya ranchi ya taifa kwa ajili ya
ufugaji wa kisasa na wa kibiashara ambao wanavitumia kinyume.na malengo ili wagawiwe wananchi.
Waziri mkuu huyo amesema wanaotakiwa kunyang’anywa
vitalu walivyomilikishwa ni pamoja na wale walioshindwa kuviendeleza na
wanaokodisha maeneo ya vitalu hivyo kwa wageni toka nje nchi wanaoingia hapa
nchini na mifugo yao,amesema wageni ndio chanzo cha migogoro kati ya wawekezaji
na wananchi, pia amepiga marufuku viongozi wa seriali ngazi za vijiji na kata
kutoa vibali kwa wageni toka nje ya nchi kwa kuwa vibali hivyo ndivyo vinawapa
uhalali wa kuingiza mifugo yao.
Kwa upande wake,waziri wa kilimo na mifugo Mwigulu
Nchemba ameeleza kuwa serikali kamwe haitamuonea mtu wakati wa zoezi la
kuwabaini wanaotumia vitalu kinyume na malengo,amesema zoezi hilo litafanyika
kwa umakini mkubwa na halitawasalimisha wanatumia vitalu hivyo kufanya shughuli
ambazo niu haramau ambazo ni pamoja na ulimaji wa bangi ukataji miti kwa ajili
ya uchomaji wa mkaa.












0 comments:
Post a Comment