Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi,na Mawasiliano,Profesa
MAKAME MBARAWA amesema Serikali imetoa Shilingi BILIONI 11 na Milioni
2 00 kukamilisha haraka ujenzi wa
Daraja la Mto Kilombero .
Daraja hilo lenye urefu wa Mita 384 linatarajiwa
kukamilika novemba 11 mwaka huu na kuepusha wananchi kupata adha ya kivuko ya
mara kwa mara inayogharimu maisha ya watu na upotevu wa mali.
Akizungumza na wananchi wa Kilombero na Ulanga
wakati akitembelea kivuko kilicho pata ajali mapema mwaka huu na kugharimu maisha
ya watu na upotevu wa mali,Profesa MBARAWA amesema serikali itahakikisha daraja
lina kw isha mapema na kuwaondolea adha wananchi wa wilaya hizo na wavuke kwa usalama zaidi .
Kwa upande wao wananchi wa Kilombero na Ulanga
wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa daraja hilo kwani kivuko kilichopo
bado si o salama na kumekuwa kukitokea
matukio mengi ya kuzama kwa kivuko n a kupoteza ndugu zao.


0 comments:
Post a Comment