Chama cha madaktari wa kinywa na meno nchini kwa
kushirikiana na wadau wengine kimefanya zoezi la uchunguzi wa afya ya kinywa na
meno pamoja na kutoa elimu kwa watoto wapatao 258 katika shule ya msingi maalum
buguruni jijini dar es salaam.
Akizungumza na itv mratibu wa zoezi hilo Bi.lizabeth
Limo amesema mbali na kufanya uchunguzi katika shule hiyo pia wanalenga
kumsaidia mtoto kutambua ni jinsigani anaweza kutunza kinywa pamoja na meno
dhidi ya magonjwa ambayo yanaweza kuepukika kwa kufuata njia sahihi katika
usafishaji.
Kwa upande wake makamu mkuu wa shule Bw,George Njau
amesema anashukuru kwa zoezi hilo kufanyika shuleni hapo kwani kutasaidia
katika kuboresha afya ya kinywa na meno kwa wanafunzi hoa na kutoa wito kwa
wadau mbalimbali katika kuwasaidia watoto wenye uhitaji maalum kwani nao wana
haki ya kupata huduma zote muhimu


0 comments:
Post a Comment