Polisi ya Uganda imetangaza kuwa
mapigano yaliyojiri magharibi mwa nchi hiyo kati ya wafuasi wa wagombea
uchaguzi wanaohasimiana ambao walishiriki katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo
yameuwa watu 22 na kuwajeruhi wengine 10.
Chama cha upinzani cha Mabadiliko ya
Demokrasia (FDC) kimeituhumu serikali ya Uganda kuwa imechochea machafuko hivi
karibuni katika eneo ambalo mgombea wa upande wa upinzani Kizza Besigye ana
uungaji mkono mkubwa dhidi ya kiongozi mkongwe Yoweri Museveni ambaye alishinda
uchaguzi wa rais uliofanyika nchini humo tarehe 18 Februari huku ukigubikwa na
udanganyifu.
Polisi ya Uganda ilisema katika taarifa
iliyotoa jana kuwa ghasia ziliibuka kati ya wafuasi wa wagombea hasimu baada ya
kufanyika uchaguzi wa serikali za mitaa katika eneo hilo tarehe 24 Februari.
Polisi imesema kuwa raia 16 waliaga dunia kwenye machafuko kati ya wafuasi wa
wagombea hao wanaohasimiana, na wengine 6 waliaga dunia baada ya polisi
kuingilia kati ili kuzima ghasia hizo. Mbali na kuuawa watu hao, watu wengine
10 walijeruhiwa wakiwemo wanajeshi wanne, huku nyumba 149 zikichomwa moto.


0 comments:
Post a Comment