
Polisi ya Uturuki Jumatatu hii,
imewakamata watuhumiwa kadhaa siku moja baada ya shambulio la kujitoa mhanaga
la bomu lililotegwa ndani ya gari, ambalo liliwaua watu wasiopungua 36 katikati
mwa mji wa Ankara, kwa mujibu wa serikali.
Waasi wa chama cha PKK wananyooshewa
kidole kuhusika na shambulio hilo.
Masaa kdhaa baada yashambulio hilo,
ndege ya jeshi la Uturuki iliendesha mashambulizi ya kulipiza kisasi katika
ngome kadhaa za waasi wa PKK katika milima ya kaskazini mwa Iraq, hasa karibu
na maeneo ya Kandil na Gara, uongozi wa jeshi la Uturuki umetangaza.
Watu wanne hadi watano wamekamatwa pia
katika mji wa Sanliurfa, Kusini-Mashariki, mji wenye wakazi wengi kutoka jamii
ya Wakurdi ambapo kulinunuliwa gari iliyotegwa bomu, ambayo ililipuka Jumapili
usiku dhidi ya basi ndogo katika eneo linalotembelewa na watu wengi la Kizilay.
Pigo hili mpya lililotokea katikati mwa
mji wa Ankara,shambulio la pili ndani ya kipindi kisizidi mwezi moja,
linamuweka hatarini Rais Recep Tayyip Erdogan, ambaye chama chake kilishinda
uchaguzi wa wabunge Novemba 1, huku akiahidi "kutokomeza" kundi
la waasi wa Kikurdi na kukabiliana dhidi ya "machafuko".
Hakuna kundi hata moja lililodai
kuendesha mashambulizi ya Jumapili usiku, lakini serikali ya Uturuki iliharakia
kuwanyooshoea kidole "magaidi" wa Kikurdi.
"Tunaamini kwamba mmoja wa
washambuliaji ni mwanamke mwenye uhusiano na kundi la PKK," amesema
kwa masharti ya kutotajwa jina afisa wa Uturuki, akiliambia shirika la habari
la Ufaransa la AFP. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uturuki, Seher Cagla
Demir, mwenye umri wa miaka 24, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Balikesir
(kaskazini magharibi), ametambuliwa kutokana na alama za vidole vyake.
Februari 17, shambulio la kujitoa mhanga
la bomu lililotegwa ndani ya gari, ambalo lilidaiwa kutekelezwa na kundi la
wapiganaji la PKK, lililolenga magari yaliokua yakiwasafirisha wanajeshi
liliwaua watu 29.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment