Serikali imesema katika kuhakikisha usawa wa
kijinsia unapatikana nchini vipo baadhi ya vipaumbele ambavyo imewiweka ili
kufikia usawa huo ikiwemo kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za
kimamuuzi pia kusimamia upatikanaji wa haki na sheria kwenye masuala
yanayowakumba wanawake.
Hayo yamesemwa na waziri wa nchi,Ofisi ya
Rais-Utumishi na Utawala bora Mh.Angella Kairuki alipokuwa akizindua kampeni
iliyoshirikisha wanawake toka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam yenye
lengo la kumsaidia Mwanamke ya namna anyoweza kujikomboa kifikra na kiuchumu
iliyoandaliwa na taasisi ya haki za wanawake ambapo amesema serikali inatambua
changamoto zinazowakabiri wakina mama wa kitanzania na hivyo itashirikiana nao
kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi.
Kampeni hiyo yenye kauli mbiu isemayo 'Mwanamke Piga
Kazi usikubali Mapenzi yakatishe ndoto zako ambapo moja kati ya mwanaharakati
wa masuala ya wanawake amewataka wanawake kuacha dhana ya kuwa tegemezi na
kupiga kazi ili kujikomboa kiuchumi.
0 comments:
Post a Comment