Image
Image

MBOWE:Migogoro,Rushwa,Utovu wa nidhamu ndivyo vilivyo tukoseha ushindi uchaguzi mkuu 2015.







Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mh.Freeman Mbowe,amesema migogoro  ndani ya chama hicho iliyosababishwa na Rushwa, utovu wa nidhamu na maadili kwa baadhi ya viongozi wake wa ngazi mbalimbali,ndiyo sababu kubwa iliyokifanya kupoteza ushindi wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.
Kauli hiyo imetolewa na Mh.Mbowe wakati akifungua kikao cha baraza kuu la chama hicho jijini mwanza, kinachohudhuriwa na wajumbe zaidi ya mia tano, mwenyekiti huyo wa chadema taifa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la hai mkoani kilimanjaro, amesema kamati kuu inapendekeza kwa baraza kuu kuundwa kwa kamati ya maadili kitaifa ambayo itakuwa chini ya makamu mwenyekiti wa chadema taifa, prof. Abdallah safari.
Mh. Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni ametumia fursa hiyo kukanusha propaganda zinazoenezwa na mahasimu wao kisiasa kwamba, aliuza chama hicho kwa aliyekuwa mgombea urais wa chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA ) Mh. Edward Lowassa.
Kwa upande wake, aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu wa oktoba 25 mwaka jana Mh.Edward lowassa, amewashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kumpigia kura, wakiwemo wale waliomfuata na kumuomba kutoa tamko kuhusu msimamo wake baada ya mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi jaji mstaafu damian lubuva kutangaza matokeo ya urais.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment