Image
Image

Nyumba nane zachomwa moto usiku wa kuamkia leo Kisiwani Pemba.



Nyumba nane zimechomwa moto usiku wa kuamkia leo Kisiwani Pemba zikiwemo nyumba za makazi,tawi la CCM Kibirinzi na kituo cha afya Kiuyu kilichokuwa kinatumika kuhifadhi dawa zilizokwisha muda wa matumizi na mali za idara ya afya.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kaskazini Pemba kamishina msadizi Hasana Nasiri ali amesema wana washikilia watu wawili kwa tuhuma ya matukio hayo huku upelezi mkali ukiwa ume anzishwa kubaini wengine.
Nae Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa Kaskaini Pemba Omar Khamis Othuman amesema kufatia matukio hayo kuanzia leo wata piga marufuku watu kuzungumza kwenye vijiwe kuanzia sambili hadi asubuhi.
 Wamiliki wa nyumba zilizo ziliokumbwa na kadhi hiyo na baadhin ya mashuhuda  walisema awali walijihisi joto kali na ghafla wakona moto unawake juu kwenye paa la nyumba ndipo walipo piga yowe kuomba msada.
Afisa mdhamini wizara ya afya Pemba Ukasha Daudi Ukasha amesema miongoni mwa hasara zilizo letwa na moto huo ni  kuteketeza vitabu vya kusomea mbali mbali vya shule ya sekondari kiuyu minungwini walivyo pewa msada vilivyo hifadhiwa ndani ya kituo hicho.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment