Mawakala sita wa pembejeo za kilimo watumbuliwa jipu
na kuu wa Mkoa wa Mvomero Bi.Betty Mkwasa baada ya kushindwa kuwajibika katika
usambazaji wa mbegu katika kata za wilaya hiyo ambapo amemuagiza mratibu wa
pembejeo wilaya kuvunja mkataba na mawakala hao na kuingia mkataba na wengine
watakao weza kuwahudumia wakulima kwa wakati.
Amewatumbua mawakala hao wakati wa kikao kilicho
shirikisha madiwani na watendaji, wenye viti wa kamati ya pembejeo mkuu wa
wilaya ya mvomero bi.betty mkwasa amesema hawezi kuwavumilia mawakala wazembe
ambao wanashindwa kufanya kazi kama walivyo ingia mkataba wa kuwahudumia
wakulima na kumlazimu kuamuru wasitishwe mkataba wao mara moja.
Nao baadhi ya watendaji na wenyekiti wa kamati ya
pembejeo kata wamesema wakulima wapo tayari kwa kilimo lakini kutokana na
ukosefu wa pembejeo kama vile mbolea za kupandia na kukuzia pamoja na mbegu
zimewafanya wakulima washindwe kuendelea na kilimo jambo ambalo linaweza
kuwasababishia baa la njaa.
0 comments:
Post a Comment