Kenya na Tanzania zimekubaliana kutekeleza miradi ya
maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu na kukuza biashara.
Katika mazungumzo ya viongozi wa nchi hizo mbili,
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameeleza kufurahishwa kuona Rais John Magufuli wa
Tanzania yupo tayari kuhakikisha nchi hizo zinakuwa karibu na miradi ya
maendeleo inaharakishwa.
Mradi mwingine wa maendeleo walio ujadili ni
kuzalisha ajira kupitia viwanda.
'' Kwa sababu nia yetu sisi ni kuona maendeleo
yatakayogusa wananchi wa kawaida, tumalize umasikini, uchumi ukue, na hivyo
hatuwezi kufanya tukiwa tumetengana'' alisema Kenyatta.
Kwa upande wake Rais Magufuli amesema Tanzania na
Kenya zina kila sababu za kuimarisha mahusiano ya kibiashara hasa katika ujenzi
wa viwanda, utakaozalisha ajira kwa kuwa watu wake ni wamoja.
''Wazee wetu mzee Kenyatta na mzee Nyerere walijenga
mazingira mazuri ya kuwa na nchi hizi mbili, wakati wakipigania uhuru, sasa
sisi vijana wetu ni wakati wetu kwenda mbele kwa ajili ya maendeleo'' alisema
Rais Magufuli.
Rais Magifuli ameutaja mradi moja wapo kuwa ni
ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tanzania kwenda Kenya kupitia
Namanga.


0 comments:
Post a Comment