Mhasibu wa Wizara ya Habari , Utamaduni, Sanaa na
Michezo Godfrey Osmund akimweleza Naibu waziri wa wizara hiyo Mhe. Anastazia
Wambura jinsi atakavyozikatia risiti fedha ambazo wadau wa michezo wamezitoa
kwa ajili ya kuichangia Timu ya Taifa ya wanawake ya Mpira wa miguu ya Twiga
Stars.
Naibu Waziri wa HabariUtamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe. Anastazia Wambura akimkabidhi leo Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey
Osmund shilingi milioni mbili zilizotolewa na Mohammed Dewji kwaajili ya
kuisaidia timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars. Hadi sasa
wadau wa michezo wameshaichangia timu hiyo shilingi milioni 17.
Picha na Anna Nkinda.



0 comments:
Post a Comment