Klabu ya Uturuki Galatasaray imepigwa marufuku ya
kutoshiriki mashindano yeyote yalioandaliwa na shirikisho la soka barani ulaya
UEFA kwa kipindi cha miaka miwili kwa kukiuka kanuni za uadilifu wa kifedha
(financial fair play).
Mabingwa hao wa soka ya Uturuki walisajili hasara kubwa
iliyolazimu UEFA kuchukua hatua baada ya ufichuzi mwezi Januari.
Galatasaray ilifuzu kwa hatua ya makundi katika
kinyang'anyiro cha kuwania kombe la mabingwa barani Ulaya msimu uliopita.
Vigogo hao wa soka ya Uturuki wanashikilia nafasi ya 5 hivi
sasa katika jedwali la ligi kuu.
Galatasaray, ambayo iliilaza Arsenal kupitia mikwaju ya
penalti katika fainali za kuwania kombe la UEFA mwaka wa 2010 wamekuwa wakifuzu
kwa mechi za kombe la mabingw barani ulaya katika misimu 4 mfululizo.
Msimu huu wanacheza katika ligi ya daraja la pili yaaani
Europa ambapo waliambulia kichapo mikononi mwa Lazio.


0 comments:
Post a Comment