Leicester wamepoteza nafasi ya kufungua mwanya wa alama tano
kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kutoka sare 2-2 na West Brom.
Salomon Rondon alimkwepa Robert Huth na kuwapa West Brom
uongozi dakika ya 11 lakini Danny Drinkwater alisawazishia Leicester.
Andy King aliwaweka Leicester uongozini lakini Craig Gardner
alisawazishia West Brom kupitia mkwaju wa adhabu.
Leicester waligonga mwamba mara mbili katika mechi hiyo
iliyochezewa uwanja wao wa nyumbani wa King Power Stadium, lakini
hawakubahatika kupata bao la ushindi.
Sare hiyo imewaacha Leicester alama tatu pekee mbele ya Tottenham
Hostspur.
Spurs wanaweza kwenda kileleni iwapo watafanikiwa kuwashinda
West Ham uwanjani Upton Park Jumatano.
Leciester wamo alama sita mbele ya Arsenal ambao watakutana
na Swansea Jumatano.
West Brom, ambao sasa wameshindwa mechi mbili pekee kati ya
10 walizocheza majuzi zaidi ligini wamo nambari 13 ligini, alama 12 kutoka eneo
la kushushwa ngazi.
Matokeo ya mechi za EPL zilizochezwa Jumanne
Aston Villa 1-3 Everton
Bournemouth 2-0 Southampton
Leicester 2-2 West Brom
Norwich 1-2 Chelsea
Sunderland 2-2 Crystal Palace


0 comments:
Post a Comment