Image
Image

Waziri wa afya apokea msaada wa fedha kwaajili ya wagonjwa wa Moyo.



WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Ally Mwalimu amepokea msaada wa fedha kwa ajili ya kuwezesha matibabu ya wagonjwa wa moyo katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo kwa msaada huo, jumla ya watoto 101, wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika taasisi hiyo kwa gharama za fedha hizo zilizotolewa na Jumuiya ya Kihindu waishio Dar es Salaam ijulikanayo kama BAPS Charity, kwa kuguswa kwao na kutoa msaada mkubwa na upendo waliouonyesha kwa watanzania wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo.
Wiziri Ummy amebainisha kuwa, kiasi cha msaada unaotolewa utawezesha wagonjwa wapato hao kupatiwa matibabu ya moyo hivyo kuwa, faraja kubwa kwa wagonjwa waliokuwa wakisubiria huduma hizo kwa muda mrefu kutokana na kushindwa gharama za matibabu yake.




Aidha, kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi amepongeza kwa msaada huo kwani utasaidia kutoa matibabu kwa watoto hao 101, huku pia taaisi yake ikikabiliwa na changamoto ya wagonjwa wengi ambapo amezitaka taasisi na wadau wengine kujitokeza kuchangia ilikupunguza wagonjwa wanaosubiria kupatiwa matibabu hasa upasuaji.
Prof. Janabi ameeleza kuwa, matibabu ya wagonjwa wa moyo yana gharama kubwa kwani kwa mtoto mmoja ndani ya nchi yanafikia hadi Milioni nne (Mil 4) huku kwa nje ya nchi matibabu hayo yakifikia hadi Milioni 16, gharama hizo ni kubwa hivyo wadau na taasisi binafsi zimeombwa kujitokeza ilikuokoa maisha ya wagonjwa wengi hasa watoto ambao wapo katika taasisi hiyo na mikoa mingine.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment