Mgombea wa Democratic Hillary Clinton na mgombea wa
Republican Donald Trump wameshinda majimbo mengi katika mchujo wa kuteua
wagombea urais Marekani katika vyama vyao Jumanne Kuu.
Wagombea wote wawili wameshinda majimbo saba kila mmoja. Wameshinda
wote wawili majimbo ya Alabama, Georgia, Tennessee na Virginia.
Bi Clinton pia ameshinda Arkansas na Texas, naye Bw Trump
akashinda Massachusetts.
Bw Trump hata hivyo ameshindwa na Seneta Ted Cruz majimbo ya
Texas, Alaska na Oklahoma.
Mgombea wa Democratic Bernie Sanders naye ameshinda kwake
nyumbani katika jimbo la Vermont, Minnesota, Colorado na pia katika jimbo la
Oklahoma.
Mchujo wa Jumanne Kuu hushuhudia majimbo 11 yakifanya mchujo
kwa pamoja huku maandalizi ya uchaguzi mkuu tarehe 8 Novemba yakiendelea
kushika kasi.
MOJA
KWA MOJA: Mchujo wa Jumanne Kuu Marekani
Bi Hillary Clinton, aliyekuwa wakati mmoja waziri wa
mashauri ya kigeni wa Marekani, pamoja na mfanyabiashara tajiri kutoka New York
Donald Trump walipigiwa upatu kushinda majimbo mengi Jumanne Kuu.
Utafiti wa maoni ya baada ya kura ulikuwa umeonyesha Trump
na gavana wa Ohio John Kasich wakikabiliana vikali katika mchujo wa chama cha
Republican jimbo la Vermont, lakini baadaye Trump aliibuka mshindi.
Bi Clinton na Bw Sanders pia walikabiliana vikali katika
jimbo la Massachusetts, kaskazini mashariki mwa Marekani lakini Clinton
akaibuka mbabe.
Matokeo kwa sasa:
• Donald Trump (Republican): Alabama, Georgia,
Massachusetts, Tennessee, Virginia, Arkansas, Vermont
• Ted Cruz (Republican): Texas, Oklahoma, Alaska
• Marco Rubio (Republican): Minnesota


0 comments:
Post a Comment