Norwich wamejipata eneo la hatari Ligi ya Premia baada ya
kushindwa na Chelsea wakiwa kwao nyumbani Carrow Road.
Norwich walilazwa 2-1 kwenye mechi hiyo iliyochezwa Jumanne
jioni, huku Chelsea wakiendelea kupanda kwenye jedwali chini ya meneja Guus
Hiddink.
Beki wa Blues Kenedy alifunga bao kwa kombora alilochomoa
akiwa hatua 20 kutoka kwa goli, baada ya sekunde 39 pekee kuchezwa.
Bao hilo ndilo la kasi zaidi kufungwa Ligi ya Premia msimu
huu.
Diego Costa aliongeza la pili sekunde chache kabla ya
mapumziko, ingawa alionekana kuotea.
Cameron Jerome aligonga mwamba wa goli kabla ya Nathan
Redmond kufunga lakini bao lake halikutosha na Norwich walishindwa mechi yao ya
nane katika mechi tisa.
Norwich wakishuka eneo la hatari, Chelsea wamepanga kwenye
jedwali hadi nambari nane, mara yao ya kwanza kuwa sehemu ya juu ya jedwali
tangu wiki ya kwanza ya msimu.
Wameenda mechi 12 ligini bila kushindwa.
Norwich watakutana na Swansea, walio alama tatu juu yao,
Jumamosi nao Chelsea wakaribishe nyumbani Stoke siku nne kabla ya kucheza mechi
ya marudiano hatua ya 16 bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Paris
St-Germain.
Matokeo ya mechi za EPL zilizochezwa Jumanne
Aston Villa 1-3 Everton
Bournemouth 2-0 Southampton
Leicester 2-2 West Brom
Norwich 1-2 Chelsea
Sunderland 2-2 Crystal Palace


0 comments:
Post a Comment