Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amenusurika kwa mara ya
pili katika kipindi cha mwaka mmoja kuondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa
na imani naye, baada ya hoja iliyowasilishwa bungeni kutoungwa mkono na wabunge
walio wengi.
Hoja hiyo ya tuhuma dhidi ya Zuma ya utendaji mbovu wa
kiuchumi iliwasilishwa bungeni na chama kikuu cha upinzani Muungano wa
Kidemokrasia (DA) na kupigiwa kura hapo jana. Hata hivyo Rais wa Afrika Kusini
alishinda hoja hiyo kutokana na uungaji mkono wa chama chake tawala cha ANC
ambacho kinahodhi karibu thuluthi mbili ya viti vyote vya bunge la nchi hiyo.
Wabunge 225 walipiga kura ya kupinga hoja hiyo ya kutokuwa
na imani na utendaji wa kiuchumi wa Zuma iliyoungwa mkono na wabunge 99 mbali
na 22 walioamua kutopiga kura. Rais wa Afrika Kusini mwenyewe hakuhudhuria
kikao hicho cha bunge.
Akizungumza katika kwa niaba ya chama kikuu cha upinzani,
Waziri kivuli wa Fedha David Maynier aliliambia bunge lililokuwa likirusha moja
kwa moja kikao hicho kupitia televisheni ya taifa kuwa Rais Zuma amekuwa
mvurugaji wa uchumi ambaye hatosita kufanya lolote ili kuweza kuendelea kubaki
madarakani ikiwemo kubomoa uchumi na kuibomoa Afrika Kusini yenyewe.
Kiongozi wa chama hicho cha Muungano wa Kidemokrasia Mmusi
Maimane alitoa wito wa kuondolewa madarakani Zuma akiashiria Waafrika Kusini
milioni nane na laki mbili ambao amesema hawana ajira.
Licha ya tuhuma hizo, Waziri wa serikali Bi Lindiwe Zulu
aliliambia bunge katika mjadala uliochukua takribani muda wa masaa matatu kwamba
Jamii ya Kimataifa ina imani na Rais Zuma.
Daryl Glaser, mchambuzi wa siasa katika Chuo Kikuu cha Wits
amesema kwa hatua yao hiyo, wapinzani wanatumai kudhoofisha nafasi ya Zuma
mbele ya umma na vilevile kuzidisha mpasuko ndani ya chama tawala


0 comments:
Post a Comment