Mahkama ya katiba nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
imeidhinisha ushindi wa rais mpya wa nchi hiyo Faustin-Archange Touadéra.
Mahakama hiyo ilitoa ripoti hiyo jana na kumtangaza
mwanasiasa huyo kuwa ni rais mpya wa nchi hiyo aliyeibuka mshindi katika duru
ya pili ya uchaguzi wa rais hapo tarehe 14 Februari. Zacharie Ndouba, mkuu wa
mahkama ya katiba ameunga mkono matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa tarehe 20
Februari na Tume ya Uchaguzi (ANE) na kusisitiza kuwa, Faustin-Archange
Touadéra ndiye rais halali aliyechaguliwa na wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya
Kati kwa kupata asilimia 62.69 ya kura dhidi ya mshindani wake Anicet-Georges
Dologuélé. Aidha imetupilia mbali maombi yoyote ya kutaka kubatilishwa matokeo
ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa nchi hiyo. Hatua hiyo imekuja baada ya
Anicet-Georges Dologuélé kutuhumu kuwepo uchakachuaji mkubwa katika uchaguzi
huo na hivyo kuitaka mahakama hiyo ya katiba kutupilia mbali matokeo hayo.


0 comments:
Post a Comment