Mamia kadhaa ya wanamgambo wa kundi la kitakfiri la Daesh
wameuawa katika mashambulio yaliyofanywa na jeshi la Syria katika viunga vya
mji wa Aleppo.
Jeshi la Syria limefanikiwa kusonga mbele katika eneo la Tal
Hammad katika kiunga cha mji wa Aleppo na kufanikiwa kuwaangamiza magaidi
wasiopungua 450 wa kundi hilo la kitakfiri.
Duru za Syria aidha zimeripoti mafanikio ya karibuni ya
jeshi katika eneo la Ghouta ya Mashariki na mashambulio ya mtawalia
yanayofanywa na magaidi katika vitongoji vya Kefraya na al- Fouaa vilivyoko
kandakando mwa mji wa Aleppo, ambavyo vingali vimezingirwa na matakfiri hao.
Magaidi 17 wa kundi la Jabhatun-Nusra wameangamizwa katika operesheni hiyo.
Wiki iliyopita raia kadhaa waliuliwa na kujeruhiwa katika
mashambulio yaliyofanywa na magaidi katika vitongoji vya Kefraya na al- Fouaa.
Makundi ya kigaidi na kitakfiri ya Daesh (IS) na
Jabhatun-Nusra ni miongoni mwa makundi ya kigaidi ambayo hayajashirikishwa
katika ustishaji vita uliotangazwa nchini Syria baina ya serikali na wapinzani;
na kwa sababu hiyo jeshi linaendeleza operesheni zake za mashambulio dhidi ya
makundi hayo.
Wakati huohuo Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema, jeshi
la nchi hiyo linaendelea kuonyesha stahamala kwa ukiukaji wa usitishaji vita
uliotangazwa nchini humo, lakini stahamala hiyo ina mpaka.
Rais Assad ameyasema hayo leo katika mahojiano na
televisheni ya Ujerumani.../
0 comments:
Post a Comment