Tanzania na Uganda zimeanza mchakato wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka
katika nchi ya Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania unaotarajiwa
kugharimu dola za Kimarekani bilioni nne.
Makubaliano ya kujengwa kwa mradi huo yalifikiwa na marais wa
nchi hizo Dr,John Magufuli wa Tanzania na Yoweri Museveni
wa Uganda walipokutana jijini Arusha wakati wa kikao cha wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mawaziri wa sekta zinazohusiana na nishati,makatibu wakuu na watendaji wa ngazi mbalimbali wa nchi za Tanzania na Uganda wamekutana jijini Arusha na kusaini
makubaliano ya kuanza kwa mchakato ambao waziri wa nishati wa Uganda
Bi.Irine Liuloni amesema mradi huo
utaongeza chachu ya uchumi kwa nchi za Afrika
Mashariki .
Aidha viongozi hao wamesema kitakachofuata baada ya hatua hiyo
ni taratibu za ndani za serikali za Tanzania na Uganda na kwamba
mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya
kimataifa ya uchimbaji wa mafuta ya total
unatarajiwa kuanza mapema mwanzoni mwa mwaka 2017.
Kama mradi huo utakamilika na kuanza uzalishaji unatarajiwa kuongeza fursa za kiuchumi na ajira kwa
wananchi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment