Mahakama ya hakimu mkazi kisutu imewahukumu raia wawili wa
china kulipa faini ya shilingi bilioni
108.7 ama kwenda jela kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo 706.
Raia hao wawili wa china, XU FUJIE na HUANG GIN wanaotetewa
na makili Edward Chuwa na Nehemia Nkoko walihukumiwa
kifungo hicho na Mh.Hakimu Mfawidhi,Cyprian Mkeha akisoma huku hiyo Mh.Mkeha
amesema mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na mashahidi tisa wa upande wa mashtaka pamoja na utetezi
wao na hivyo kuwakuta washatakiwa hao na makosa kadhaa.
Hakimu akaongeza kuwa
kwa kuzingatia hali halisi ya kesi,ushahidi na hasara ambayo taifa imeipata kutokana na
tembo 226 kupoteza maisha kwa kuuwa ni
wazai kuwa raia haoa wa wachina
wanatakiwa kupatiwa adhabu kama hiyo.
Akiendelea kuisoma hukumu hiyo, hakimu Mkeha amesema ametoa
adhabu hiyo pia kwa kuzingatia uzito wa maombi ya mawakili wa serikali,Faraja Nchimbi
Paul Kadushi na Wankyo Simon na maombi
ya utetezi kuwa wapunguziwe adhabu.
Awali kabala ya huku hiyo mawakili wa serikali,nchimbi aliiomba
mahaka iwape adhabu kali washtakiwa hao kwa kuwa kati ya kipindi cha 2010
na desemba 2013 hapa chini jumla ya tembo 892 waliuawa .
Alidai kuwa washtakiwa hao waliingia nchini 2010 hadi
novemba 2013 walipokamatwa kwa makosa hayo na kuwepo rumande
matukio ya mauaji ya tembo yalipungua.
Nchimbi alibainisha kuwa washtakiwa hao waliiua robo ya
tembo wanaouawa hapa nchini na kwamba kutokana na wingi wa nyara walizokutwa
nazo inaonekana wazi ni miongoni mwa vinara wakubwa , wawezeshaji na wahusika
wa shughuli za ujangili zinaeoendelea
hapa nchini.
Novemba 2, 2013 katika mtaa wa kifaru mikocheni kinondoni
washtakiwa hao wanadaiwa kukamatwa wakiwa na nyara hizo za serikali ambazo ni
vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 1,880 na thamani ya sh
5,435,865,000 wakivimiliki bila ya kuwa na
kibali kutoka kwa mkurugenzi wa wanyamapori.
0 comments:
Post a Comment