Zikiwa zimebaki siku mbili kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa marudio
visiwani Zanzibar chama cha wananchi CUF kimeendelea na msimamo wa kutoshiriki
uchaguzi huo na kuwataka wanachama na wafuasi wa chama hicho kujiepusha na
mikusanyiko isiyo ya lazima kwa kukaa majumbani mwao ili kuondokana na vurugu
zinazoweza kusababishwa na wahuni dhidi ya wananchi wasio na hatia.
Akizungumza na waandishi wa habari naibu katibu mkuu wa CUF Zanzibar
Bwana.Nassoro Mazrui amesema chama cha CUF hakijaweka wakala katika ngazi
yoyote ya uchaguzi huo na kuwataka wafuasi kutambua swala la kupiga kura hakuna
anaweza kulazimishwa.
0 comments:
Post a Comment