Mwenyekiti wa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Jaji Damian
Lubuva amewataka wananchi wa Zanzibar kutembea kifua mbele na kwenda kutimiza
haki yao ya kikatiba kupiga kura hapo kesho kwa ajili ya kupata viongozi wa
kuwaongoza.
Jaji Lubuva ameyasema hayo baada ya kuwepo kwa woga miongoni
mwa baadhi ya wananchi kwa kuwepo kwa vikosi vya ulinzi na usalama katika
maeneo mengi jambo ambalo baadhi ya wananchi wamekuwa wakihoji juu ya kuwepo
kwa nguvu kubwa kiasi hicho.
''Usalama upo wa kutosha na suala la kuwepo kwa wanajeshi
Zanzibar si suala geni katika mambo ya uchaguzi wa mataifa mbalimbali lengo ni
kulinda amani na usalama wa wananchi hivyo wananchi wasitilie shaka wajitokeze
bila uoga''-Amesema Jaji Lubuva.
Uchaguzi wa marudio Zanzibar unarudiwa kesho tarehe
20.03.2016 baada ya uchaguzi wa awali wa tarehe 25.10.2015 kufutwa na tume ya
uchaguzi Zanzibar kupitia kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jecha Salum Jecha kwa
vigezo kadhaa kikiwepo cha upinzani kujitangazia ushindi mapema kinyume na
sheria.
0 comments:
Post a Comment