Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bibi
Nkosozana Dlamini Zuma amekaribisha uamuzi wa Ghana wa kutoa visa kwa watu
kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika wakati wanafika Ghana.
Rais John Dramani Mahama wa Ghana alitangaza uamuzi
huo wakati akilihutibia bunge Februari 25. Alisema kuanzia mwezi Julai mwaka
huu, Ghana itawaruhusu watu kutoka nchi zote wanachama wa Umoja wa Afrika
kuingia Ghana na kupewa visa ya muda wa siku 30, uamuzi aliosema utahimiza
usafiri wa ndege, biashara, uwekezaji na utalii.
Bibi Zuma amepongeza uamuzi wa Ghana uliopitishwa na
baraza la utendaji la Umoja wa Afrika mwanzoni mwa mwaka huu. Bibi Zuma amesema
anatarajia kuwa nchi nyingine za Afrika zitafuata hatua ya Ghana, ili kuhimiza
mafungamano, maendeleo na amani barani Afrika.


0 comments:
Post a Comment