Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa
na serikali za mitaa Mh.George Simbachawene amewataka wakuu wa mikoa nchini
kubadilika kwa kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea kwavile kila serikali
inayoshika madaraka ina utaratibu na utamaduni wake bila kujali uzoefu wa mtu
kwavile kila zama na kitabu chake.
Mh.Simbachawene ameyasema hayo jijini Dar es Salaam
wakati akizungumza na wakuu wapya wa mikoa nchini pamoja na kuwataka kusimamia
mamlaka za serikali za mitaa kwa kusimamia kila kinachotokea kila siku badala
ya kuwaachia makatibu tawala wa mikoa Mh.Simbachawene amewakumbusha wakuu hao
kuwa timu ya awamu ya tano chini ya rais Mh.John Pombe Magufuli kuwa mfumo
uliopo si wa kuchezea.
Awali akimkaribisha waziri kuzungumza na wakuu hao
naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa
Mh Selemani Jaffo aliwataka wakuu hao kusimamia ukusanywaji wa mapato katika
kila halmashauri zao sambamba na kutimiza wajibu wao kikazi na usimamizi wa
miradi ya maendeleo ya wananchi.
Halikadhalika katika kikao hicho wakuu hao
waliagizwa kusimamia haki za wanawake hususani katika masuala ya ardhi ili haki
itendeke mabaraza ya ardhi ngazi za vijiji hadi kata ikibidi yavunjwe na
kuangaliwa upya ili haki itendeke na mwenendo mzima wa mabaraza ya ardhi ya
wilaya ufuatiliwe upya ili wenye nacho
na wasionacho wapate haki sawa ambapo baadhi ya wakuu hao walikuwa na haya ya
kusema.
0 comments:
Post a Comment