WATU watano wamefariki dunia huku nane wamejeruhi,
katika ajali iliyoyahusisha magari manne, mawili yakiwa katika msafara wa
Kamati ya Bunge Utawala na TAMISEMI maeneo ya Kerege, Bagamoyo Pwani, anaandika
Mwandishi Wetu.
Waliofariki katika ajali ni Hilda Msele (59), Mkuu wa Idara
ya Mipango ya Uchumi, Makame Ally (40), Dereva wa Tasaf, Khalid Hassan (40),
Tunsime Duncan, Mwanasheria wa Wilaya na Ludovick Palangya, Mchumi.
Majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Taifa ua Muhimbili
ni Ibrahim Matovu, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bagamoyo, Juliana Msaghaa,
Mhandisi wa Maji wilaya, Dorothy Njetile, Mratibu wa Tasaf, George Mashauri,
Mweka Hazina wa Wilaya, Amadeus Mbuta, Mshauri wa Tasaf, Julius Mwanganda, Mkuu
wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Tauliza Halidi, Mwananchi na Amari Mohamed,
Mwananchi.
Aliyepelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo na
kuruhusiwa ni George Mbilinyi ambaye ni Afisa Utumishi na Utawala wa Wilaya.
Ajari hiyo iliyohusisha lori la mchanga, gari dogo
yaliyokuwa yanatokea Bagamoyo kuja Dar es Salaam, na magari mawili yaliyokuwa
kwenye msafara wa Kamati hiyo, yaliyokuwa yanaenda Bagamoyo kwa shughuli zake
za kibunge.
Magari yaliyokuwa katika msafara wa kamati hiyo, ni gari la
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) na gari la Mkurugenzi wa Wilaya ya
Bagamoyo ambayo yaligongwa na lori hilo la mchanga na kusababisha vifo vya watu
hao na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Ajali hiyo ilitokea baada ya gari dogo lililokuwa linatokea
Bagamoyo kupunguza mwendo ghafla na kusababishwa lori lililokuwa nyuma yake
kuligonga na kuhama upande wa pili na kuyagonga magari mawili yaliyokuwa katika
msafara wa kamati ya Bunge.
0 comments:
Post a Comment