Saidi Msangi,Dar es Salaam.
Serikali imewasimamisha kazi maafisa 3 wa jeshi la
kikosi cha zimamoto kwa tuhuma za kushiriki wizi wa mafuta ya ndege na mmoja
kati yao kuiba mizigo ya wateja kwa kushirikiana na wafanyakazi wa kampuni ya
swissport.
Akizungumza katika ziara ya kushitukiza aliyoifanya
katika viwanja vya ndege vya Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es Salaam naibu
waziri wa wizara ya mambo ya ndani Mhe.handisi Hamad Masauni amewataja walio
simamishwa kazi ni ALFANI KISANA na MUSSA MANDAULI ambao walikamatwa na madumu
10 ya mafuta ya ndege wakiwa na gari la serikali lenye usajiri STJ 2948 huku
askali mwingine aliye julikana kwa jina la ABIAS Mwanza akishutumiwa kwa kosa
la kushirikiana na mfanyakazi wa swissport lucas maganda kwa kosa la kuiba
mzigo abiria.
Akiwa katika kiwanja hicho Mhe.Masauni amekagua
utendaji kazi katika idara ya uhamiaji,polisi na jeshi la zimamoto na kuagiza
viongozo wa idara hizo zilizopo chini ya wizara yake kufanya kazi kwa uaminifu
na yeyote atakaye kiuka atua kali zitachukuliwa dhidi yake.
0 comments:
Post a Comment