WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewasili jijini Mwanza jana
jioni tayari kuanza ziara ya kikazi ya mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita kuanzia
leo.
Alitua kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza saa 11:40 jioni na
kupokewa na viongozi mbalimbali, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa
Mulongo.
Baadaye alikagua vikundi vitatu vya ngoma.
Aidha mamia ya wananchi walijipanga kwenye barabara ya
Airport, kumlaki Waziri Mkuu huku baadhi yao wakiwa na mabango yenye ujumbe
tofauti kwenda mjini kumlaki.
Hii ni mara ya kwanza kwa waziri huyo kutua Kanda ya Ziwa
tangu ateuliwe kuwa Waziri Mkuu wa 11 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri Mkuu ataanza ziara mkoani Simiyu, akianzia wilayani
Busega. Atakapomaliza ziara hiyo mkoani Simiyu ataenda mkoani Kagera na Geita
kwa muda wa siku 14.
0 comments:
Post a Comment