NAPE Nnauye, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na
Michezo anatarajia kuwa mgeni rasmi katika shindano la urembo la Miss Tanzania
2016 katika Hoteli ya Ramada Resort jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo utawakutanisha wadau mbalimbali wa
tasnia ya urembo wakiwemo wabunifu wa mavazi, mawakala wanaoandaa mashindano ya
Miss Tanzania na wakurungenzi wa kampuni mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo
Hashim Lundega, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International
Agency amesema, uzinduzi huo utakuwa wa aina yake na kwamba, burudani kadhaa
zitakuwepo.
“Mara tu baada ya uzinduzi huu katika Jiji la Dar es
S alaam utahamia Mkoa wa Arusha ambako pia kutakuwa na aina
nyingine ya uzinduzi,” amesema Lundega
0 comments:
Post a Comment