Baadhi ya wanasiasa wakongwe pamoja na wachambuzi
mbalimbali waliozungumza na mtanzania, walieleza kusikitishwa na uamuzi wa rais magufuli, wakisema ni wa kukurupa
huku wengine wakipongeza hatua hiyo.
Sumaye.
waziri mkuu mstaafu, frederick sumaye alisema
kilango hakuwa na hatia kiasi hicho kwa sababu bado hajaujua vizuri mkoa huo.
“ukweli haiwezekani rc asimamie jambo hilo muda
mfupi na hata akipewa miezi sita akakague watu hao ‘physically’ bado haitoshi.
“kama aliletewa taarifa kuwa kuna watumishi hewa na
yeye akasema hakuna…hapo kuna tatizo. lakini ndio hivyo kila mtu na utawala wake,
kumwajibisha mtu ambaye hata huo mkoa na ofisi hajaijua vizuri kwa kweli
inasikitisha. hii haijapata kutokea popote na si kitu cha kawaida,”alisema
sumaye.
Prof baregu.
kwa upande wake, mjumbe wa kamati kuu ya chama cha
demokrasia na maendeleo (chadema), profesa mwesiga baregu alisema kuna udhaifu
mkubwa wa namna ya kuwapata wakuu wa mikoa, wilaya na makatibu wakuu.
profesa baregu aliyepata kuwa mjumbe wa iliyokuwa
tume ya mabadiliko ya katiba, alisema nafasi hizo zimekuwa zikitolewa kisiasa
na ndio maana kumekuwapo na matatizo ya mara kwa mara kwa sababu viongozi hao
hawajachekechwa.
“hizi nafasi zilipaswa zipatikane kwa usaili yaani
watu waombe au wapendekezwe halafu ndio wapewe nafasi hizo, lakini nafasi hizo
zimekuwa zikitolewa kisiasa ndio maana haya yote yanatokea,”alisema msomi huyo.
alisema kosa la pili alilolifanya rais magufuli, ni
namna alivyotoa maagizo wakati kuna vyombo na taasisi zinazohusika katika
uchunguzi, badala ya wakuu wa mikoa ambao hawana utaalamu wowote.
“kwanini hakutaka kutumia vyombo vya ukaguzi na
badala yake anawaambia wakuu wa mikoa? tuna ofisi ya cag na pale kuna watumishi
wengi wa ukaguzi wangeenda wilayani na mikoani kufanya uchunguzi lakini
kuwaachia marc ambao wengine ni walewale waliokuwepo katika baadhi ya
mikoa…yaani ajikague mwenyewe halafu akuletee?
“rc hajui jinsi ya kuhesabu…katika hili rais
magufuli amekurupuka kwa sababu kazi hiyo ilipaswa kufanywa na vyombo husika
viandae taarifa kitaalamu. sasa kwa sababu na yeye kilango alipewa nafasi hii
kisiasa naye anakubali na hana namna.
“bado kazi ya ukaguzi kwa watumishi hewa
haijafanyika ipasavyo, mpaka likifanyika kitaalamu ndio tutaelewa kwa sababu
wapo ambao si hewa lakini wameunganishwa,”alisema profesa baregu.
Wasira.
mwanasiasa
mkongwe aliyepata kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, steven wasira alisema
alichokifanya rais magufuli ni kawaida kwa sababu kila kiongozi ana aina yake
ya uongozi.
“lakini hata wakati wa nyerere (mwalimu julius)
jambo kama hili lilitokea, kuna mtumishi mmoja simkumbuki kwa jina aliteuliwa
na baadaye ikabainika hana sifa akatenguliwa ndani ya muda mfupi. lakini hili
ni jambo la rais yeye ndiye ana mamlaka ya kuteua na kutengua,”alisema wasira.
Msekwa.
kwa upande wake, mwanasiasa mkongwe na spika
mstaafu, pius msekwa alisema kila zama na kitabu chake na kwamba haiwezekani
kuufananisha uongozi wa magufuli na viongozi waliopita.
“ni sahihi alichokifanya rais kwa sababu ndio
‘style’ yake ya uongozi na yeye ndio mwenye mamlaka ya kuteua na
kutengua,”alisema.
Dk.Bisimba.
naye mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki
za binadamu (lhrc), dk. hellen kijo bisimba alisema pamoja na kasi ya rais
magufuli, lakini hajamtendea haki kilango kwa sababu bado alikuwa mgeni katika
mkoa huo.
“huyu alikuwa ndio amefika tu na pengine watendaji
ndio waliomdanganya sioni sababu ya yeye kuwajibishwa. angepewa hata onyo kuwa
awe mwangalifu zaidi.
“na kwa mtazamo wa kijinsia tunaweza kudhani labda
kwa sababu ni mwanamke kwani hata rais anaweza kupewa taarifa za uongo na watu
wa chini yake, lakini hatutamtoa madarakani,”alisema dk. bisimba.
Prof. Mpangala.
mhadhiri wa chuo kikuu kishiriki cha ruaha (ruco),
profesa gaundence mpangala alisema alichokifanya rais magufuli ni hatua za
kinidhamu kwa watumishi wa serikali na kwamba wengine wajifunze.
bana.
naye mhadhiri wa chuo kikuu cha dar es salaam
(udsm), dk. benson bana alisema alichokifanya rais itakuwa fundisho kwa
viongozi waliopewa dhamana.
Machali.
aliyekuwa mbunge wa kasulu mjini, moses machali,
aliandika kupitia ukurasa wake wa facebook akimpongeza rais magufuli kwa hatua
aliyoichukua.
“kiukweli,
salute kwako ‘mr president’ kama kweli inavyoripotiwa mitandaoni kwamba
umetengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa shinyanga ambaye ni mteule wako, tena wa
juzi juzi tu, si jambo jepesi kwa kiongozi kumwadabisha mteule wake hapa afrika
na hasa tanzania.
“naanza kuiona tanzania mpya na kuamini uliyowaasa
wateule wako mbalimbali, tukio hilo litaongeza umakini na kuwafanya wakuu wa
mikoa na wateule wengine serikalini kujenga tabia ya kufuatilia au kufanya
uchunguzi au utafiti wa masuala yanayopaswa kutekelezwa na wao… keep it up mr
president,” alisema machali.


0 comments:
Post a Comment