Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John William Kijazi
Muda Mfupi baada ya kuapishwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John William Kijazi aliwakumbusha Makatibu hao kuwa kiapo hicho kinaashiria kufanya kazi kwani wapo wengi lakini wao wameaminiwa na kuteuliwa hivyo nivyema wakazingatia kanuni na masharti mbalimbali.
“Fomu mliyo saini muizingatie na muisome kwa mara ya pili mjue miiiko ya uongozi ipoje kwani ipo humo kwani mkizingatia naamini hakutakuwa na matatizo katika utendaji kazi wenu.
Balozi Kijazi amesema kuwa endapo wakati wakutekeleza majukumu yao yakazi watazingatia hiyo miiko itakuwa rahisi mnoo kuhakikisha kuwa suala la rushwa linalokuwa likitajwa kunyemelea baadhi ya maeneo basi watakuwa wakwanza kuhakikisha wanalikemea katika ngazi ya Mikoa mpaka Wilaya wanayoenda kuifanyia kazi na kuhakikisha kuwa wanafanya kazi na wakuu wa mikoa kwa uwiano mzuri bila kuvutana wakati nyumba wanayojenga nimoja.
“Mkaripoti kwenye vituo vyenu vya kazi sasa, sitegemei Migogoro mtakayoikuta muipige chenga muishughulikie,muangalie inamuda gani mtakapoona imewashinda ndipo mnaileta kwetu tuishughulikie”Alisema Balozi Kijazi.
Aidha amewaambia Makatibu Tawala hao wa Mikoa kuwa kiapo hicho ni sehemu ya imani kwa kila muda na kila wakati wawe wanakikumbuka kusudi kiwe chachu ya kuwafanya wao wafanye kazi kwa weledi katika mikoa waliyopangiwa,Pia amewapongeza kwa kuteuliwa.
Wakati wa kiapo hicho Serikali imetakiwa kutoa elimu kuhusu suala la Mgongano wa kimaslahi kwa viongozi na watendaji wa Serikali ili waweze kutenda kazi zao kwa kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma.
Baada ya zoezi hilo la kuapishwa kwa makatibu Tawala wa Mikoa wapya wapatao kumi Kamishna Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma Jaji Salome Kaganda akamtaka Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi kutoa semina elekezi kwa makatibu tawala wa Mikoa walioteuliwa na rais ili kuepuka kile alichokiita kutumbuliwa kutokana na wengi kuponzwa na suala la Mgongano wa Kimaslahi.
Awali kamishna mkuu wa sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma Jaji Salome Kaganda aliwalisha kiapo cha pamoja cha maadili ya viongozi wa Umma Makatibu tawala wote kumi waliopishwa na rais hii leo.
0 comments:
Post a Comment