Aliyekuwa
kiongozi wa waasi wa Sudan ya Kusini Bwana RIEK MACHAR hatimaye
ameapishwa kuwa makamu wa rais wa kwanza nchini humo katika serikali
mpya ya umoja.
Akizungumza baada ya kuapishwa amesema wakati umefika
kuwaleta pamoja watu wa nchi hiyo ili waungane na kwamba ingawa kutakuwa
na changamoto lakini moyo wa kisiasa utatua changamoto zote hizo kwa
njia ya maridhiano.
Kwa upande wake Rais SALVA KIIR alisema amani ndiyo njia pekee ya nafuu kwa
wananchi wa Sudan ya Kusini kuondokana na mateso ya vita visivyostahili vilivyowakumba kwa zaidi ya miaka miwili.
Bwana
KIIR amesema anaamini hiyo ndiyo njia pekee ya kurejea katika njia ya
amani, utulivu na ustawi wa nchi hiyo ya Sudan ya Kuaini ambayo ni
changa zaidi duniani.
Home
Kimataifa
Slider
MACHAR hatimaye ameapishwa kuwa makamu wa rais wa kwanza nchini Sudan ya Kusini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment