Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai
Mkoani Kilimanjaro limewafukuza kazi watumishi wake sita na kuwashusha vyeo na
mishahara watumishi watano baada ya kubainika na tuhuma za wizi, kujipatia fedha
kwa njia ya udanganyifu na kuidhinisha malipo ya fedha bila idhini.
Maamuzi hayo yametolewa na baraza hilo katika kikao
maalum baada ya kuridhishwa na taarifa ya kamati mbili za uchunguzi baada ya
kusimamishwa kazi mwezi Novemba Mwaka Jana na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri hiyo Bw.Saidi Mderu kupisha uchunguzi.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bi. Helga Mchomvu
amewataja waliofukuzwa kazi kuwa ni
maafisa utumishi wawili, mchumi, wahasibu wawili na dereva mmoja ambaye
katika mazingira ya kutatanisha alinunua dawa hewa za Hospitali teule ya Machame
yenye thamani ya shs.32.7mil.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw Mderu
amesema, tuhuma hizo ziligunduliwa na mkaguzi wa ndani wa Halmashauri yake Bw.
Maiko Mosha na kufanyiwa kazi na tume hizo ambazo ziliongozwa na Bi. Grace
Makiluli katibu tawala msaidizi wa sekritarieti ya mkoa wa Kilimanjaro.
Baada ya kubainika kwa tuhuma hizo baraza hilo
limempongeza mkaguzi huyo kwa kufanya
kazi kwa uadilifu mkubwa kwa kuwa angeweza kudanganyika kwa kutumia fedha hizo.
Mkuu wa wilaya ya hai Bw.Gelaswus Byakanwa
amelipongeza baraza hilo kwa hatua hizo
na kueleza kuwa kazi kubwa ya
Madiwani ni kusimamia mali na raslimali
za Serikali ili wananchi wapate huduma bora za serikali yao ya awamu ya tano
ambayo ina dhamira ya kuwahudumia.
Source:Itv.
0 comments:
Post a Comment