Beki wa Liverpool Mamadou Sakho anachunguzwa na UEFA kwa
kufeli ukaguzi wa madawa ya kulevya.
Ijapokuwa raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26
hajapigwa marufuku rasmi, hatashiriki mechi yoyote wakati uchunguzi huo unapoendelea
kulingana na Liverpool.
BBC radio 5 inasema kuwa Sakho alipatikana na dawa za
kusisimua misuli baada ya mechi ya UEFA kati ya Liverpool dhidi ya Manchester
United.
Sakho aliyesajiliwa kwa pauni milioni 18 kutoka Paris
St-Germain mwaka 2013 amecheza mechi 34 msimu huu ikiwemo mechi 10 katika ligi
ya Yuropa.
Alifunga katika ushindi wa Liverpool wa 4-3 dhidi ya
Borussia Dormund mnamo tarehe 14 mwezi Aprili na kufuzu katika nusu fainali ya
kombe hilo.
Liverpool ambayo ni ya 7 katika jedwali la ligi ya Uingereza
inaialika Newcastle siku ya Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment