Lionel Messi amefikisha magoli 500 tangu aanze
kucheza soka, baada ya kufunga goli moja jana lakini halikutosha kuisaidia
Barcelona kupata ushindi baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa
Valencia.
Kwa kipigo hicho Barcelona inaweka rekodi mbaya ya
kufungwa mara tatu mfululizo katika Ligi ya Hispania La Liga, ikiwa ni mara ya
kwanza kupata kichapo cha mfululizo cha namna hiyo tangu mwaka 2003.
Goli la mpira uliogongwa na Ivan Rakitic uliotokana
na krosi ya Guilherme Siqueira uliingia wavuni na kujifunga kabla ya baadaye
Santi Mina kumalizia shambulizi hatari na kuandika bao la pili kwa Valencia
katika kipindi cha kwanza.
MSN wakiwa hawaamini matokeo
Ivan Rakitic akimfunga kipa wake kimakosa




0 comments:
Post a Comment