Serikali ya Jamhuri ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wake wa kutumia bandari ya Tanga nchini Tanznaia kusafirishia mafuta yake ghafi kwenda nchi za nje.
Taarifa iliyotolewa na serikali jijini Dar es Salaam imesema uamuzi huo umetangazwa na Rais YOWERI MUSEVENI wa Uganda wakati wa mkutano mkuu wa 13 wa ushoroba wakaskazini uliomalizika jijini Kampala nchini Uganda.
Ujumbe wa Tanznaia uliokamilisha mazungumzo hayo na hatimaye kushuhudia kutangazwa kwa hatua hiyo uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa DR. AUGUSTINE MAHIGA
Uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini unaendelea na kukamilisha mpango huo wa bomba la mafuta ambao pia utanufaisha nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati.
Makamu wa Rais wa kampuni ya Total Afrika Mashariki Bwana JAVIER RIELO alishakutana na Rais JOHN MAGUFULI na wakaafikiana kwamba ujenzi wa bomba hilo linalokadiriwa kuwa la urefu wa kilomita 1,410 uanze haraka iwezekanavyo.
Kampuni ya mafuta ya Total ndiyo inayofadhili ujenzi huo na inatarajia kutumia dola za Kimarekani karibu bilioni 4 ambazo tayari zimeshaandaliwa.

0 comments:
Post a Comment