Chad imeongeza kwa miezi sita hali ya hatari iliyowekwa kwenye ukanda wa Ziwa Chad kukabiliana na mashambulio ya mpakani ya wapiganaji wa Nigeria wa kikundi cha Boko Haram.
Radio ya Chad imesema wabunge kwa kauli moja azimio la kuongeza muda huo wa hali ya hatari ambao umekuwa ukitumika tangu tarehe 9 Novemba mwaka jana.
Waziri wa Usalama Bwana AHMAT MAHAMAT BACHIR amesema hatua hiyo itasaidia kutumika kupunguza uwezo wa wa mapigano ya kikundi hicho cha Boko Haram nchini Chad.
Katika miezi ya hivi karibuni mashambulio ya mpakani ya wapiganaji wake yamepungua ya mwisho yakiwa mawili ya kujitoa mhanga maeneo ya Guite na Miterine katika ukanda wa Ziwa Chad ambapo watu watatu waliuawa na wengine 56 kujeruhiwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment