Jumuiya ya Afrika Mashariki imezitaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuiga mfumo wa utatuzi wa migogoro unaotumiwa na Serikali ya Tanzania wa kutumia nguvu kubwa ya ushawishi,na mazungumzo kuondoa chochoko zinazoweza kusababisha umwagaji wa damu usio wa lazima badala ya kusubiri kutumia nguvu hizo madhara yakishatokea.
Changamoto hiyo im etolewa na Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo,Dakta.RICHARD SEZ I BERA alipokuwa akizungumza na makundi mbalimbali ya wananchi na watendaji waliojitoka kuwakumbuka Mamilioni ya wananchi waliopoteza ma isha katika mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994 .
Wakizungumza mwishoni mwa hafla hiyo washiriki kutoka nchi mbalimbali,wakiwemo walionusurika kwenye mauaji hayo ya kimbari na mengine yanay osababishwa na masuala ya siasa katika nchi zao ambao walifanya maandamano na kuweka mashada ya maua katika mnara ulioko kwenye Makao Makuu ya jumuiya hiyo wameishukuru Tanzania kwa kuwa kuwa jirani mwema na kimbilio la wote wenye shida.
Kwa upande wake mwakilishi wa Serikali ya Tanzania katika hafla hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,WILSON NKAMBAKU amesema lengo la Tanzania ni kuona wananchi wa nchi zote wanaishi kwa amani.
.
Home
News
Slider
EAC yazitaka nchi mwanachama wa jumuia hiyo kuiga utatuzi wa migogoro kutoka Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment