Kamanda mmoja wa ngazi ya juu wa kundi la Al-Shabaab
amejisalimisha kwa jeshi la Somalia kwenye kijiji kilicho karibu na mji wa
Galcad, katikati ya Somalia.
Kamanda wa jeshi la taifa la Somalia kwenye sehemu
hiyo kanali Ahmed Mohamed amesema, kamanda huyo, Ahmed Mohamud Afrah amekubali
msamaha na kujisalimisha kwa serikali ya Somalia.
Afrah aliwahi kuwa kamanda wa kundi la Al-Shabaab
aliyeshughulikia kukusanya kodi kwenye sehemu hiyo.


0 comments:
Post a Comment