Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imempa dhamana
Mtuhumiwa Isaac Abakuki anayetuhumiwa kumtukana Rais John Magufuli kupitia
kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.
Hakimu mfawidhi Agustino Rwezire amesema Mahakama
baada ya kupitia hoja mbili
zilizotolewa na upande wa mashtaka na
mshtakiwa, imeridhia kutoa dhamana kama haki ya msingi ya mshtakiwa kutokana na
kosa alilotenda ambapo dhamana hiyo ni ya Wadhamini wawili waliotakiwa kuwa na
jumla ya shilingi milioni tano.
Kwenye siku ya kwanza kufikishwa Mahakamani Polisi
walisema Tarehe 17 March 2016 Isaac Abakuki akiwa nyumbani kwake Olasiti Arusha
alipokea ujumbe kwenye account yake ya Facebook ukisema ‘mnamlinganishaje
Magufuli na Nyerere’ ukiwa ni Ujumbe wa mjadala ulioanzishwa kwenye mtandao wa
kijamii kufuatia hatua ya Rais Magufuli kupiga simu kwenye kipindi cha Clouds
360 CloudsTV na kuwapongeza Watangazaji wa kipindi hicho.
Baada ya kusoma huo ujumbe Mtuhumiwa aliandika
comment kujibu alichokisoma na kuandika >>> ‘Hizi ni siasa za maigizo
halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere wapi
buana“….. comment ya mtuhumiwa iliwaudhi na kuwakwaza watu wengi
walioona Facebook na wakaamua kufikisha malalamiko yao kwa mamlaka ya
mawasiliano Tanzania TCRA. – Polisi


0 comments:
Post a Comment