Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kamwe
hataruhusu raia wake kukabidhiwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya
Jinai ICC kutokana na vurugu zilizotokea kwenye uchaguzi wa mwaka 2007- 2008,
zilizosababisha vifo vya watu 1,200 na wengine laki 6 kupoteza makazi yao.
Akihutubia mkutano wa hadhara mjini Nakuru, Rais
Kenyatta amesema ushirikiano wa miaka mitano kati ya Kenya na ICC umekwisha, na
sasa Kenya itatatua matatizo yake kwa kutumia mahakama zake. Mkutano huo
ulihudhiriwa na naibu rais Bw William Ruto, mwanahabari Joshua Sang, na maofisa
wengine ambao ICC ilifuta kesi zao.
Kauli ya Rais Kenyatta imekuja wakati ICC imetoa
hati ya kuwaita mahakamani raia wengine watatu wa Kenya kujibu tuhuma za kuingilia
kesi ya Bw Ruto na Bw Sang.
Ingawa Kenya inabanwa kisheria kushirikiana na ICC,
wabunge wa nchi hiyo wametishia kuiondoa Kenya kwenye mahakama hiyo.


0 comments:
Post a Comment