Image
Image

Kesi ya uchaguzi Nyamagana Mabula ashinda kesi dhidi ya Wenje Leo.

Mahakama kuu kanda ya Mwanza imeifuta kesi ya kupinga Matokeo ya Ubunge katika jimbo la Nyamagana iliyokuwa imefunguliwa na mbunge aliyemaliza muda wake Ezekiel Wenje (Chadema) baada ya kushindwa kuthibitisha.
Kufutwa kwa Kesi hiyo kumeweza kumpatia ushindi Stanslaus Mabula (CCM) kuwa mbunge halali wa jimbo la Nyamagana jijini Mwanza,ambapo wafuasi wa CCM wanaelezwa kuwapo nje ya Mahakam hiyo huku wakishangilia ushindi wa Mbunge huyo.
Mwaka jana Octoba 25 Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stanslaus Mabula alitangazwa mshindi wa mbio za ubunge katika jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza kwa kupata kura 81, 170 dhidi ya Ezekiel Wenje (Chadema) aliyepata kura 79, 280.
Taarifa zaidi Tutawaletea.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment