Benki ya dunia imeidhinisha mkopo wa dola milioni 65 za kimarekani kwa ajili ya kuboresha ufanisi na uwazi kwenye huduma za mahakama nchini Tanzania.
Taarifa iliyotolewa na Benki hiyo inasema pesa hizi zinaendana na mahitaji ya mpango wa maendeleo kuelekea mwaka 2025, na mkakati wa kuboresha mahakama za nchi hiyo. Taarifa hiyo imesema Tanzania inahitaji kuboresha maisha ya watu wake kwa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, kuongeza uwazi na kupunguza umasikini. Taarifa pia imesema tofauti ya mapato imeongezeka kutokana na fursa chache za ajira, uhaba wa huduma na utoaji mbaya wa huduma hasa katika maeneo ya vijijini.
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa kanda ya Afrika Mashariki Bella Bird amesema kwa watanzania wengi huduma za mahakama ni anasa, lakini haitakiwi kuwa hivyo, kwa kuwa ni msingi wa jamii endelea na maisha ya watu.
Home
News
Slider
Benki ya dunia yaidhinisha dola milioni 65 kwa ajili ya kuboresha huduma za mahakama Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment