Burundi inaendelea kutengwa kimataifa baada ya Umoja wa Ulaya kusimamisha katikati ya mwezi Machi msaada wake wa kifedha kwa Burundi, Jumuiya ya nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa (OIF) imesitisha ushirikiano wake na nchi hiyo Alhamisi hii.
Burundi haifutwi katika Jumuiya. Lakini IOF inabaini kwamba Bujumbura haijaonyesha nia njema ili kumaliza mgogoro unaoendelea nchini humo na kuamua kukaidi kutekeleza mapendekezo yanayotolewa na nchi viongozi mbalimbali duniani wakiwemo wafadhili wake.
Hali ya usalama ambayo inaendelea kuzorota siku hadi siku, haki za binadamu zinakiukwa na bado hakuna ishara yoyote ya kuanza kwa mazungumzo ya kisiasa na upinzani. Yote hayo yamesababisha Jumuiya ya nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa (OIF) kupaza sauti na kusitisha ushirikiano wake na Burundi Alhamisi hii.
"Uamuzi huu unafuatia uamuzi wa Baraza la Kudumu la Jumuiya hiyo mwezi Julai mwaka jana, ambapo iliiweka Burundi chini ya uangalizi kufuatia uchaguzi wa Rais Nkurunziza, Louis Hamann, msemaji wa Katibu Mkuu wa OIF amesema. Uamuzi wa (Alhamisi) una lengo la kuongeza shinikizo kwa serikali ya Burundi kurejesha hali ya usalama, pia kuanza kwa mazungumzo ya kisiasa ya kweli yenye umoja ili kuondokana na mgogoro huo. "
Adhabu hii haihusu mipango inayowanufaisha moja kwa moja raia bila kupitia katika akaunti za serikali au ile ambayo iyonaweza kusaidia "kurejesha demokrasia." Kwa upande mwingine, OIF imesitisha utetezi wake kwa Burundi na Benki ya Dunia kama inavyofanya mara nyingi. Kama Umoja wa Ulaya kabla yake, IOF inatarajia kuona majibu kutoka Bujumbura wakati ambapo hazina za serikali zimesalia patupu na utabiri wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwa mwaka huu ni majanga.
Hata hivyo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo imekuwa kwa muda mrefu imetengwa nataasisi za OIF baada ya mapinduzi ya mwezi Machi 2013, hatimaye imerejeshwa rasmi Alhamisi hii katika Jumuiya hiyo kufuatia uchaguzi wa rais na ule wa wabunge uliofanyika katika " mazingira ya kuridhisha. "
Home
Kimataifa
Slider
OIF yasitisha ushirikiano wake na Burundi kufuatia mgogoro unaoendelea nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment