Serikali ya Uganda imemwonya balozi wa Marekani nchini Uganda Bw. Deborah Malac kuacha kukosoa ushindi wa rais Yoweri Museveni kwenye uchaguzi uliofanyika mwezi Februari.
Msemaji wa serikali ya Uganda Bw. Ofwono Opondo amesema Bw. Deborah Malac aliendelea kukosoa kinachodaiwa kuwa ukiukaji wa taratibu kwenye uchaguzi mkuu. Bw. Opondo pia amesema baadhi ya makundi nchini Marekani na katika Umoja wa Ulaya, wakiwemo wajumbe wao nchini Uganda waliendelea kutoa fedha kwa makundi ya upinzani ili "kusababisha mapinduzi haramu dhidi ya serikali".
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment