Umoja wa Afrika jana ulifanya shughuli za maadhimisho ya miaka 22 ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda katika makao makuu yake mjini Addis Ababa.
Kwa mujibu wa Umoja wa Afrika, lengo la maadhimisho hayo ni kuwakumbusha watu wa Afrika na jumuiya ya kimataifa kuhusu thamani ya maisha na ubinadamu, na kusisitiza ahadi ya kulinda haki za kimsingi za binadamu.
Kwenye hotuba yake, kamishna anayeshughulikia mambo ya siasa wa Umoja wa Afrika bibi Aisha Abdullahi amesisitiza haja ya kukumbuka jambo hilo kupitia kupambana na itikadi ya mauaji ya kimbari.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment